Mark 10:13-16

13 aWatu walikuwa wakimletea Isa watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wake wakawakemea. 14 bIsa alipoona yaliyokuwa yakitukia, akachukizwa. Akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa wale walio kama hawa. 15 cAmin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.” 16 dAkawachukua watoto mikononi mwake, akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.

Kijana Tajiri

(Mathayo 19:16-30; Luka 18:18-30)

Copyright information for SwhKC